GPL iko tayari kumlipa kiasi
cha shilingi Milioni mia tano, mnenguaji wa Bendi ya Twanga Pepeta,
Aisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’ ikiwa atatoa uthibitisho kwamba,
picha za utupu alizopigwa nchini Afrika Kusini ni za kutengenezwa, soma
data chini.
Ofa hii imekuja siku mbili baada
ya gazeti moja la michezo na burudani linalotoka mara mbili kwa wiki,
toleo la Jumanne Mei 18, 2010 kuchapisha makala kuhusu Aisha akikanusha
kuwa, picha zile si zake na kwamba zilitengezwa na mbaya wake kwa lengo
la kumchafua jina.
...kulia kwake ni unga..bila shaka ulimpotezea kumbukumbu
Hata hivyo, katika makala hayo,
Aisha alishindwa kuthibitisha picha hizo ni za kutengeza, zilitengnezwa
wapi na lini na vigezo gani vinavyoonesha picha hizo ni za kutengeneza.
Ushahidi wa Global kuwa, picha hizo ambazo za mnato na video ni za Aisha mwenyewe upo wazi na hakuna shaka yoyote.
Moja ya ushahidi huo, katika
picha za video, kuna sehemu Aisha anaongea kwa tambo akiwaponda watu
wanaomfuatafuata na kumsema vibaya.0
...sasa hapa inakuwaje picha hizi zikitoka gazetini...!!!!
Tunamnukuu: “Wanasema eti
nimeishiwa, nimekosa nauli ya kurudi Tanzania, waende basi kwa huyo Asha
Baraka wakaseme, maana wamezidi kwa maneno.”
Hata hivyo, sehemu kubwa ya picha
za mnato na video hizo zinaonesha wazi kwamba, Aisha alikuwa tayari
kupigwa picha hizo, kwani kuna wakati alikuwa akitazama kamera na
nyingine akiwa ameweka pozi.
......aaa jamani...niacheni ki mpango wangu!!!!
Aidha, ushaidi mwingine kuwa
picha hizo ni Aisha, mara baada ya kutua Bongo akitokea Afrika Kusini,
alimwangukia bosi wake, Asha Baraka akimwomba radhi kwa yote
aliyoyafanya Afrika Kusini ambapo gazeti hili liliripoti likiwa na
kichwa cha habari; NATESEKA.
Katika habari hiyo, Asha Baraka
‘Iron Lady’ alinukuliwa akisema kuwa, anaamini Aisha aliteleza na hivyo
ameamua kumsamehe na kumrudisha kundini kuendelea kupiga mzigo kama
kawa.
....ntajua ntakachowaeleza watanzania....
Tunamnukuu Asha Baraka: “Mimi kwa
Aisha ni kama mama au dada yake, na ninavyojua, mtoto anapojisaidia
kiganjani mzazi huwezi kuukata mkono bali utausafisha kisha kuyaacha
mambo yaendelee. Vivyo hivyo kwa Aisha, kafanya kosa lakini hakuna kosa
lisilostahili msamaha, kwahiyo asamehewe.
“Atakachokifanya Aisha ni kuomba
radhi kwa mashabiki wake na katika kila sehemu ambayo tutafanya shoo
atafanya hivyo kabla ya kuanza kutumbuiza.”
.......ni mzimu wangu tu huu...siyo mimi..!
Pia, katika kuonesha ubinadamu,
mwisho wa habari hiyo Mhariri aliwaomba Watanzania wasahau yaliyopita
kuhusu Aisha na aombewe kwa Mungu ili amwepushe na mitihani mingine
nkatika maisha yake.
Katika hali ya kushangaza sana,
baada ya kimya cha muda mrefu, Aisha ameibuka katika gazeti hilo akidai
kwamba picha zile zilikuwa za kutengeneza hali iliyozua maswali miongoni
mwa wasomaji wetu.
Habari hiyo, ambayo ilionekana
Aisha alikuwa amelenga kuwafanya Watanzania waamini Ijumaa linaandika
habari za ‘mezani’ alisema, yupo mwanaume mmoja aneyemsumbua kimapenzi
kwa muda mrefu, ambaye ndiye aliyemfanyia unyambisi huo.
......mimi siyo Aisha niangalieni vizuri...!!!!!
“Huyo anayenichafua alikuwa
ananitaka kimapenzi nikamkatalia na siwezi kumkubalia, hata kwa mtutu
simpi mwili wangu ng’o, kuamua kunitangazia sifa chafu si suluhisho la
mimi kumkubali, zaidi ya kumuona kichekesho kwani katika jamii ya watu
wastaarabu hafai, namfananisha na ‘nungayembe’ la kiume,” alisema Aisha
katika sehemu ya habari hiyo.
Aidha, aliongeza: “Picha za ngono
zilizoenea kila kona ya nchi, zinazonihusu mimi si za kweli, amefanya
hivyo kwasababu ‘nilimpiga za uso kavukavu bila chenga’, siwezi kupoteza
muda wangu kubishana naye, nitakuwa nampandisha chati, lakini ajue hata
kwa mtutu hapati kitu kwangu.”
Katika juhudi za kulishusha
‘grade’ gazeti hili, sehemu ya habari hiyo ilisomeka, ‘Anadai amekuwa
akikabiliwa na tuhuma za kupiga picha za ngono na utupu zilizosambazwa
sehemu mbalimbali hasa katika magazeti ya udaku, ambapo kiuhalisia si
zake.
....baada ya mitungi, mikasi....Aisha akiwa na Khumalo
Katika hatua nyingine, mapema
wiki hii, kijana Khumalo aliyefanya naye uchafu huo nchini Afrika
Kusini, amelitumia waraka pepe (e-mail) gazeti hili akiomba msahama kwa
Aisha.
Alisema anakiri kumtenda vibaya
(kupiga na kulikisha picha hizo) mnenguaji huyo, lakini anamuomba
amsamehe na waanze ukurasa mpya
0 comments:
Post a Comment