Ni wiki nyingine tena tunakutana kupitia safu hii nikiamini umzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kilasiku kama kawaida.
Mimi mzima na bado naendelea kuzungumzia mapenzi, mapenzi haya haya ambayo yamekuwa yakiwaliza baadhi ya watu kila kukicha.
Wapo wanaojuta kupenda lakini mbaya zaidi wapo wanaolia kwa sababu ya vitu vidogo vidogo ambavyo vimekuwa haviwaendei sawa katika uhusiano wao.
Ni jambo lililo wazi kwamba, usaliti umekuwa ukiwatesa wengi tena ukijaribu kuchunguza sababu za baadhi ya watu kuwasaliti wapenzi wao, kutoyajua mapenzi yale ya faragha ni moja wapo.
Mimi mzima na bado naendelea kuzungumzia mapenzi, mapenzi haya haya ambayo yamekuwa yakiwaliza baadhi ya watu kila kukicha.
Wapo wanaojuta kupenda lakini mbaya zaidi wapo wanaolia kwa sababu ya vitu vidogo vidogo ambavyo vimekuwa haviwaendei sawa katika uhusiano wao.
Ni jambo lililo wazi kwamba, usaliti umekuwa ukiwatesa wengi tena ukijaribu kuchunguza sababu za baadhi ya watu kuwasaliti wapenzi wao, kutoyajua mapenzi yale ya faragha ni moja wapo.
Wapo
wasichana au niseme wanawake ambao kimaumbile wana mvuto sana.
Wamejaaliwa uzuri wa sura na kila kitu kiasi cha kutamaniwa na kila
mwanaume wanayekutana naye.
Lakini
linapozungumziwa suala la mapenzi kwa mwanamke, wanaume wanaangalia
vitu vingi, achilia mbali hilo la muonenako, pia wanaangalia utundu na
ubunifu wa faragha. Hapo ndipo panapowakosesha raha baadhi ya wanawake
wazuri.
Wanakuwa
ni wenye kupata bahati ya kupendwa lakini hao hao ndiyo wale ambao kila
siku wanaachwa. Si jambo la ajabu huko mtaani kukutana na msichana
mkali ile mbaya lakini akawa si mtu wa kutulia na mwanaume kwa muda
mrefu, kwanini? Kwa sababu hayajui mapenzi.
Ni tatizo siriasi?
Msichana mzuri aliyeumbika kutoyajua majamboz ni tatizo na ndiyo maana anaweza kuwa mtu wa kulia kila siku.
Anaweza
kukumbana na malalamiko kutoka kwa mpenzi wake kwamba anachokipata ni
tofauti na alivyotarajia. Hakuna kinachowauma walio wengi kama kusikia
kutoka kwa wapenzi wao kuwa hawawaridhishi.
Kwa
maana hiyo ni tatizo siriasi lakini lina ufumbuzi wake. Hakuna
aliyezaliwa na kuanza kutembea moja kwa moja, vile vile kuingia kwenye
uhusiano ukawa hujui lolote siyo tatizo ila unachotakiwa kukifanya ni
kujifunza.
Zungumza na wataalam wa masuala ya mapenzi, soma vijarida na magazeti, naamini utapata elimu tosha ya kuweza kumfanyia mpenzi wako yale yatakayomfurahisha.
Ugoigoi
faragha kwa mwanamke ni chanzo cha wengi kusatiliwa, tena utasalitiwa
zaidi kama kila siku utakuwa ni mtu yule yule, yaani hujifunzi chochote.
Mwanamke lazima awe mbunifu kwa mpenzi wake, abuni mbinu za kumdatisha
ili kuhakikisha haachwi kirahisi.
Unapobaki kujisifia kuwa wewe ni mzuri wakati huna mashamsham yoyote itakuwa ni kazi
bure. Matokeo yake sasa utashangaa mpenzi wako anakwenda kwa mwingine
ambaye ukimuangalia na kujilinganisha na wewe, unaanza kujiuliza, hivi
alichokifuata kwa yule ni nini?
Hakuna
kingine, kafuata majamboz. Ndiyo maana nikasema, uzuri wako kama hujui
chochote faragha, ujiandae kusalitiwa kila siku na mwisho wake utaachwa.
Ni majamboz tu?
Sifa
za mwanamke anayeweza kutulia kwenye uhusiano ukiachilia mbali uzuri wa
sura na umbo, tabia njema nalo ni jambo la msingi. Kama umzuri,
unayajua mambo ya chumbani ile mbaya ila huna tabia njema, ni tatizo.
Waswahili wanasema, tabia njema ni silaha.
Ushauri wangu
Ili
uyafurahie maisha yako ya kimapenzi, hakikisha unakuwa imara kila
idara. Kwanza mpende mpenzi wako kwa maana halisi ya kumpenda halafu
jitahidi kumpatia furaha ya kweli.
Miongoni
mwa mambo yanayoweza kumfurahisha mpenzi wako ni kumshibisha pale
mnapopeana chakula cha usiku, ale ashibe na wewe ushibe, mtadumu.
Mbinu
za kumshibisha mpenzi wako, zipo nyingi ila kwa kuwa ukurasa huu
unasomwa na watu wa kila rika, siwezi kuandika wakati huu.
0 comments:
Post a Comment