HTML Table

TANZIA...MUIGIZAJI MAARUFU WA ISIDINGO LETTIE MATABANE ALIYEKUWA AKIISHI NA VIRUSI VYA HIV AFARIKI DUNIA LEO


Lesego Motsepe (Lettie Matabane), enzi za uhai wake

Mwaka 2011 Lettie aliwahi kujitangaza kuwa anaishi na Virusi vya Ukimwi


Aliyekuwa muigizaji maarufu katika Tamthilia ya Isidingo The Need ya Afrika Kusini, Lesego Motsepe maarufu zaidi kwa jina la Lettie Matabane, amefariki dunia nchini mwake Afrika Kusini mapema leo. 
Lettie, ambaye alijipatia umaarufu mkubwa katika tamthilia hiyo kuanzia mwaka 1998 hadi 2008 alipoamua kuondoka, alikuwa akiishi na virusi vya Ukimwi kwa zaidi ya miaka 15. Mwaka 2011, aliwashitua mashabiki wake baada ya kuwatangazia kuwa yeye ni muathirika wa ukimwi. Hata hivyo wengi walimpongeza kwa kuwa na ujasiri wa kujitangaza hadharani, kwani kwa miaka mingi alikuwa akifanya kazi ya ubalozi wa mambo ya ukimwi. Aliianza kazi hiyo ya ubalozi kabla hajaathirika na hata alipoathirika hakushituka sana ingawa hali hiyo ilibadili maisha yake kabisa.
Tamthilia ya Isidingo ni miongoni mwa tamthilia kongwe na maarufu nchini Tanzania ambayo imekuwa ikioneshwa na televisheni ya ITV kwa zaidi ya miaka kumi sasa bila kuchosha watazamaji wake.

Mungu ailaze roho yake mahala pema - AMEEN!
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment