Niwape hi kwa furaha sana wapendwa
wasomaji wa safu hii, ingawa zaidi ningependa ziwafikie wanafunzi popote
pale gazeti hili linaposomwa. Hawa jamaa ni wadau wangu wakubwa sana,
hasa katika kubadilishana mawazo inapobidi. Juzi
nilikuwa naperuziperuzi kwenye mtandao, mara nikakutana na picha za
aibu zilizopigwa na msichana ambaye ametambulishwa kama ni mwanafunzi,
haikuelezwa kama ni denti wa sekondari au vyuo, lakini kwa uzoefu,
inaonekana kabinti ni ka sekondari! Nilipoziona,
zikanikumbusha miaka kadhaa nyuma, kama minne au mitano hivi, wakati
picha za msichana mmoja, aliyekuwa amevalia fulana zinazotumiwa na shule
moja ya sekondari iliyopo Mbezi, jijini Dar es Salaam, zilipovuja na
kufika gazetini. Binti huyo, alipigwa picha akiwa katika mikao
mbalimbali akiwa mtupu!
Simulizi zilivuja kwamba kabla ya picha hizo kufika magazetini, ambako zilichapishwa, msichana huyo alishajaribu mara nyingi kuzuia zisisambae lakini bila mafanikio. Unajua ilikuwaje? Mtu wa kwanza kuzidaka, alimfuata na kumuonyesha picha zake na kumtisha kuwa angezipeleka magazetini au kwa wazazi wake kama asingempa uroda. Kwa hofu, denti akalazimika kutii matakwa yale. Basi ikawa mchezo, picha zikaendelea kuhama kutoka kwa huyu hadi huyu na binti akajikuta akigeuka mtumwa wa ngono ili kulinda heshima yake, hadi alipokuja kugundua kuwa angetumika hadi mwisho wa dunia, akaamua kukataa, akisema liwalo na liwe, ndipo zilipofika gazetini na kutoka! Kuna jambo moja la dhahiri kupitia kwa yule dada, kwamba alijuta na alifahamu kwamba alifanya makosa kupiga picha zile, ambazo kwa vyovyote alifanya hivyo akiwa na akili timamu kwani zote alionekana akiichekea kamera. Kama asingejuta, asingekubali kuwaziba watu midomo kwa njia ya kuutoa mwili wake kwa watu asiowafahamu. Nimeanza na mchapo huo kama kuwaweka sawa ili muweze kunielewa ninachotaka kuwaambia na ambacho nyinyi wanafunzi, hasa wa kike, mtambue na kuchukua hatua ikibidi.
Utandawazi katika dunia ya sasa imeufanya ulimwengu kuwa mdogo unaofanana na kiganja. Simu za mikononi ni kila kitu, unazungumza na mwenzako aliye popote, unaingia mtandao wowote wa internet, unatuma au kupokea picha, sauti na kila unachokijua. Kwa maana hiyo, mtu mmoja anaweza kupiga picha akiwa Mbinga, kisha dakika moja baadaye akaonekana katika mtandao wa Facebook, Twitter, Instragram au popote na kujikuta picha hiyo ikionekana dunia nzima. Wimbi la wadada kujipiga picha za utupu limeibuka upya na baadhi ya wanafunzi wamejikuta wakiingia mkenge. Ni hivi, wale akina dada, wakiwemo wasanii nyota wasiojitambua, wanapiga picha na kuziweka mitandaoni kwa ajili ya kujiuza. Yes, wanajiuza, tunajua! Lakini napata taabu kidogo na wewe mwanafunzi kwa kufanya vitendo hivi. Unapiga picha hizo ili iweje anko? Unajiuza, kwa nini? Kati ya watu ambao nafsi zitawashtaki baada ya kuwa zimewasuta sana, ni wanafunzi wanaojaribu kuingia katika ujinga huu. Ni punguani tu anaweza kukubali utupu wake uonekane dunia nzima. Madenti ni lazima wawe tofauti, waonyeshe kwa nini wao wanachukuliwa kuwa ni wasomi. Kujipiga picha hizo na kuzitupia kwenye mitandao, ni kuonyesha kuwa kiwango cha kufikiri ni sawa na cha wale machangudoa wa Uwanja wa Fisi, Manzese Dar , ambao hawana mbadala wa kufanya zaidi ya kuuza miili yao. Madenti wengi wanapigana picha za utupu na wengine hadi video. Huenda hufanya hivyo kwa kujifurahisha, lakini unapovua nguo na kumruhusu mtu akufotoe, ni zaidi ya kujifurahisha. Ninaogopa kama picha zako zitavuja na kumfikia mtu mwenye VVU, ambaye atakuahidi kutozipeleka magazetini kama utampa uroda. Huoni kama unajiua mwenyewe?
Tafakari, chukua hatua!

0 comments:
Post a Comment