
Ilisemekana kuwa baada ya maji kuzidi unga, mwongozaji wa filamu hiyo, Leah Ndemesamkye ‘Lamata” ilibidi ashikwe na kigugumizi baada ya kuona mauzauza hayo ya Kajala na kumuuliza ni kitu gani ambacho kimempata kwani kila anachoongea naye, yeye anaishia kucheka mfululizo.
Baada ya gazeti hili kupata habari hizo lilimvutia waya Kajala ili kudhibitisha madai hayo ambapo Kajala alikiri kulewa kidogo na kumtupia mpira rafiki yake kipenzi Wema kuwa ndiye aliyemnywesha.
Alisema: “Unajua nini, siku hiyo tulilala kwa Wema, ndiye aliyeninywesha pombe lakini mbona kazi iliendelea kama kawaida jamani?”
0 comments:
Post a Comment